Daniel 8:15-18

15 aMimi Danieli nilipokuwa ninaangalia maono na kujaribu kuelewa, mbele yangu alisimama mmoja aliyefanana na mwanadamu. 16 bKisha nikasikia sauti ya mwanadamu kutoka Mto Ulai ikiita, “Jibraili, mwambie mtu huyu maana ya maono haya.”

17 cAlipokuwa akikaribia pale nilipokuwa nimesimama, niliogopa, nikaanguka kifudifudi. Akaniambia, “Mwana wa mwanadamu, fahamu kuwa maono haya yanahusu siku za mwisho.”

18 dAlipokuwa akinena nami, nilikuwa katika usingizi mzito, huku nimelala kifudifudi. Ndipo aliponigusa na kunisimamisha wima.

Copyright information for SwhKC